Rais Samia: Wawekezaji mali zenu zipo salama

HomeKitaifa

Rais Samia: Wawekezaji mali zenu zipo salama

Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi usalama wa mali zao na hivyo wasisite kuja kuwekeza Tanzania.

Amesema hayo wakati akizindua kiwanda cha nne kwa ukubwa Afrika cha kuzalisha vioo kilichopo katika wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

“Napenda kutumia fursa hii kuwahakikishia makampuni yote yaliyowekeza Tanzania kutoka ndani na nje ya nchi kwamba mali zenu zipo salama na kwamba Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa biashara zenu kufanikiwa.” amesema Rais Samia.

Ameongeza kwa kusema kwamba Serikali yake ya awamu ya sita imefanya maboresho mengi ya kisera, kisheria na kanununi ili kuhakikisha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini yanaendelea kuwa bora zaidi.

Aidha, Rais Samia amewataka wawekezaji kuendelea kutekeleza takwa la kisheria la mpango wa urithishwaji wa ujuzi kwa wazawa kama ilivyobainishwa katika sheria ya ajira na mahusiano kazini ili kuwasaidia watanzania wengi kupata ujuzi na ajira lakini pia itasaidia mwekezaji kupunguza gharama za kuajiri wataalamu kutoka nje

 

error: Content is protected !!