Mwaka Mmoja bila Magufuli

HomeKitaifa

Mwaka Mmoja bila Magufuli

Leo Watanzannia wanaadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Dk John Joseph Pombe Magufuli aliyefariki Machi 17, 2021, huku wakishuhudia mabadiliko mbalimbali chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu aliyechukua jukumu la kuliongoza taifa bila kutarajia.

Kwa mwaka mmoja huyo, Watanzania hawawezi kumsahau Magufuli katika mambo mbalimbali aliyokuwa akitilia kama yafuatayo.

Kodi

Magufuli alikuwa akisisitiza sana katika ulipaji wa kodi ili nchi iweze kuendeshwa vizuri na miradi kusonga mbele. Alishawahi kusema kuwa,

“Niwaombe basi Watanzania tujitahidi kulipa kodi, tukifanya hivyo, sisi wenyewe tutamudu kuteleza miradi mikubwa ya maendeleo,” – Dk. John Pombe Magufuli.

Rushwa

Alikemea vitendo vya rushwa na kuahidi kuwakamata kuwafikisha kwenye mamlaka husika wale wote watakao shiriki katika vitendo hivyo.

“Nataka wala rushwa wengi wafungwe..Hilo mimi nalitaka. Najua maneno kama haya watu hawataki kuyasikia,”- Dk John Pombe Magufuli.

Kufanya kazi kwa bidii

Alikuwa na msemo wake maarufu wa hapa kazi tu na kweli kazi aliifanya hata kusisitiza wananchi hasa vijana kufanya kazi kwa bidii.

“Hatuwezi kuwa na vijana ambao wanatakiwa kuwa ndio waendesha nchi hii wakawa kila mmoja ni ulevi na madawa ya kulevya,”- Dk John Pombe Magufuli .

“Nahimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo kwa taifa letu…,”- Dk John Pombe Magufuli.

Uzalendo 

Alikuwa ni mzalendo wa taifa lake na kukiri kwamba anajenga nchi ambayo vizazi vya baadae vitakuja kunufaika nayo na ndio maana hakuacha kufanya kazi kwa bidii.

“Hili taifa letu sisi wote, tunatengenezea maisha vijana wetu na wajukuu zetu . Kwa sisi ambao tuna umri karibu miaka 60 na kuendelea hatutengenezi kwa ajili yetu, ni lazima tutengeneze mazingira ya watu wetu wasiendelee kuwa watumwa,”- Dk John Pombe Magufuli.

Hayo ni baadhi ya mambo machache aliyokuwa akisisitiza Hayati Magufuli.

 

 

error: Content is protected !!