Serikali yapiga ‘stop’ mikopo ya halmashauri

HomeKitaifa

Serikali yapiga ‘stop’ mikopo ya halmashauri

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezielekeza halmashauri zisitishe utoaji wa fedha za mikopo kwa vikundi vya wanawake , vijana na watu wenye ulemavu zinazotokana na makusanyo ya kuanzia Aprili hadi Juni mwaka huu.

Waziri Mkuu amelieleza Bunge kuwa mikopo hiyo inasitishwa ili kuipa fursa serikali kujipanga kuwa na mfumo mpya wa kuitoa.

Alisema jana wakati akihitimisha mjadala kuhusu hoja ya makadirio na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake na mfuko wa Bunge kwa mwaka 2023/2024.

Mhe. Majaliwa alisema kumekuwa na malalamiko kuhusu kiasi kidogo cha fedha za mikopo kinachotolewa kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu.

“Aidha, kumekuwa na changamoto kwenye baadhi ya halmashauri kutoa fedha hizo kwa watumishi wa halmashauri au wakati mwingine vikundi hewa badala ya walengwa na kusababisha fedha za mikopo hiyo kutorejeshwa,” alisema Majaliwa.

Aliongeza: “Nazielekeza halmashauri kote nchini kusitisha utoaji wa fedha za mikopo hiyo zinazotokana na makusanyo ya kuanzia Aprili hadi Juni, 2023 wakati serikali inajipanga kuwa na mfumo mpya wa utoaji wa mikopo hiyo.”

Pia Waziri Majaliwa amewaelekeza wakurugenzi wa halmashauri waheshimu na kuzingatia vipaumbele vinavyopitishwa na kamati ya mfuko wa jimbo.

error: Content is protected !!