Aomba talaka baada ya kunyimwa unyumba

HomeKitaifa

Aomba talaka baada ya kunyimwa unyumba

Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Halis Mbwagolo (44) ambaye ni mkazi wa Dodoma, amemfikisha mahakamani mumewe  Denis Nyoni (49) akidai talaka baada ya kutelekezwa kwa muda wa miaka 10 na kunyimwa tendo la ndoa.

Mdai huyo aliiomba Mahakama ya Mwanzo Mjini Mbeya, kuvunja ndoa yake kwa madai mume wake amemtelekeza tangu mwaka 2011 ambapo baada ya kufanya uchunguzi alibaini ana mwamake mwingine ambaye amezaa naye watoto watatu.

“Mheshimiwa hakimu, mimi nilikuwa namvumilia mwenzangu nikijua majukumu ya kazi yamembana, kumbe ana mwanamke na tayari wameshazaa watoto watatu, wakati mimi nina mtoto mmoja, kiukweli nimeumia sana,” alidai Mahakamani hapo.

Hakimu Miriam baada ya kusikiliza upande wa mdai, alimuuliza mdaiwa kama madai hayo ni ya kweli ambapo mdaiwa sio ya kweli na hayupo tayari kutoa talaka kwa sababu bado anampenda mke wake.

Mdaiwa alisema ni kweli amezaa watoto watatu, lakini haimaanishi kwamba kamuoa bali atatunza watoto kuendelea na kuendelea na ndoa yake, na yupo tayari kuhama Mbeya kumfuata mkewe Dodoma.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu, kwa ajili ya kutolewa hukumu.

error: Content is protected !!