Kampeni za uchaguzi zamponza msanii, ajitoa tuzo za AFRIMMA

HomeBurudani

Kampeni za uchaguzi zamponza msanii, ajitoa tuzo za AFRIMMA

Mwanamuziki Slapdee ametumia ukurasa wake wa Facebook kuomba radhi kwa waandaji wa tuzo za AFRIMMA na kuomba kutolewa kwenye tuzo hizo.

Slapdee amefanya uamuzi huo kutokana na mashabiki nchini Zambia kuandaa kampeni mtandaoni kuhamasisha kutokumpigia kura na badala yake wanataka kumpigia kura rapa maarufu kutoka Afrika Kusini, Cassper Nyovest.

Wafahamu wasanii ambao Diamond anashindana nao AFRIMA 2021

Slapdee, Cassper Nyovest pamoja na wasanii wengine wanaowania tuzo ya msanii bora wa kiume ukanda wa Kusini mwa Afrika.

Kampeni ya kumpinga Slapdee imekuja baada ya msanii huyo kuimba katika mikutano ya kampeni ya chama tawala cha zamani za nchini Zambia ambacho kilishindwa uchaguzi Agosti mwaka huu.

error: Content is protected !!