Polisi wakamata bangi ndani ya gereza

HomeKimataifa

Polisi wakamata bangi ndani ya gereza

Bangi zenye thamani ya shilingi milioni 1.8 zimekutwa ndani ya gereza kwenye mji wa Empangeni nchini Afrika Kusini baada ya polisi kufanya msako mkali ndani ya gereza hilo saa tisa usiku.

Polisi walioshiriki kwenye msako huo wamekuta simu 37, chaji za simu, masufuria na bangi hizo ndani ya gereza hilo la Qalakabusha.

Polisi wamesema kwamba wataendelea kufanya misako ya kushtukiza ndani ya gereza hilo kwani wamebaini kuna uhalifu unafanyika na wafungwa kumiliki vitu ambavyo haviruhusiwi.

error: Content is protected !!