Rais Samia azindua kiwanda cha nne kwa ukubwa Afrika

HomeKitaifa

Rais Samia azindua kiwanda cha nne kwa ukubwa Afrika

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kuzalisha vioo kilichopo katika wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kinachotarajiwa kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 1,000.

Kiwanda hicho lichozinduliwa leo Septemba 20,2023 ni cha nne kwa ukubwa barani Afrika kikitarajiwa kuzalisha tani 700 za vioo zitakazotumika katika nchi zote za Afrika Mashariki na Kati.

Rais Samia Suluhu Hassan akizindua Kiwanda Cha Kutengeneza Vioo Cha Sapphire Glass Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani leo Septemba 20,2023.

Asilimia 25 ya Vioo vinavyotengenezwa na kiwanda vitatumiwa katika soko la ndani huku asilimia 75 zikitarajiwa kutumika katika soko la nje hatua inayotajwa kuongeza pato la taifa.

Akizungumza katika uzinduzi wa kiwanda hicho Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema kiwanda hicho kikikamilika kitatengeneza vioo vya magari na kutengeneza ajira nyingi kwa vijana.

“Kiwanda hiki kimetengeneza ajira za watoto wa kitanzania 750 lakini tutakapo hitimisha kuwekeza kwenye laini zote tatu tutaweza kuajiri watoto wa kitanzania 1,650,” amesema Waziri Kijaji.

Kiwanda Cha Kutengeneza Vioo Cha Sapphire Glass Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani.

Aidha, Waziri Kijaji ameomba wananchi wanaokaa eneo la Engaruka walipwe fidia ili wahame katika eneo hilo kwani ndio lenye malighafi.

error: Content is protected !!