Kilichomtesa Rais wa UAE kwa miaka 8

HomeKimataifa

Kilichomtesa Rais wa UAE kwa miaka 8

Rais Sheikh Khalifa bin Zayed al-Nahyan wa Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates) amefariki dunia hii leo akiwa na umri wa miaka 73.

Kwa miaka nane sasa tangu 2014 al-Nahyan amekuwa akiugua kiharusi na hivyo kusherehekewa kama Rais wa nchi hiyo huku shughuli zote za nchi zikiwa mikononi mwa kaka yake Mohamed bin Zayed al-Nahyan.

Familia ya al-Nahyan ni moja ya falme tajiri duniani wakiaminika kuwa na utajiri wa dola bilioni 150 ($150bn)

Pamoja na kuwa rais wa UAE, Sheikh Khalifa alikuwa mtawala wa Abu Dhabi, mji mkuu wa utajiri wa mafuta wa falme saba zinazojumuisha UAE.

Kwa kutumia katiba ya UAE Makamu wa Rais wa sasa wa nchi hiyo, Sheikh Mohammed bin Rashid al-Maktoum atakuwa Rais wa mpito hadi hapo Baraza la shirikisho linalojumuisha watawala wa falme zote saba watakapokutana ndani ya siku 30 kumchagua rais mpya.

Falme zinazounda UAE ni Abu Dhabi, Fujairah, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Umm Al Quwain na Ajman

error: Content is protected !!