Mbinu 4 za kujizuia kufika kileleni mapema kwa Wanaume

HomeElimu

Mbinu 4 za kujizuia kufika kileleni mapema kwa Wanaume

Wanawake wengi wanagombana na wenza wao na hata wengine kufikia hatua ya kusaliti mahusiano yao kwa sababu hawavutiwi kuwaona waume zao wakiwahi kufika kileleni huku wao wakiwa bado hawajapata dozi inayotesheleza. Tatizo kubwa linalowasumbua wanaume wengi wenye tatizo la kufika kileleni mapema ni kuwa na pupa na haraka ya kufanya mapenzi.Wengi wao hupokea hisia zilizokuzwa na kwenda nazo katika ufanyaji wa tendo la ndoa.

Hizi hapa njia nne za kumfanya Mwanaume achelewe kufika kileleni:

 1.  Fanya maandalizi ya kutosha
  Ni muhimu sana kumuandaa mpenzi wako kabla ya kuanza kufanya “tendo”. Kamwe usikurupuke tu na kutaka kuanza tendo ikiwa mwenza wako akiwa tayari kwani hili linaweza kukusababisha wewe kumaliza wakati mwenzako akiwa ndio anajiandaa kuanza. Tambua kuwa maandalizi yatasaidia kufanya mhemko wako ushuke, kukuongezea kujiamini na pengine kukuwezesha wewe na mwenza wako kuanza na kumaliza safari kwa pamoja.
 2. Idanganye akili yako
  Idanganye akili ni lazima ili kuzima taarifa za juu za uzuri wa mwanamke unayefanya nae tendo, hii itasaidia “effects” za uzuri wa maumbile na raha ya starehe isipokelewe kwa nguvu kubwa mwilini. Ukifanikiwa hili basi hata mwitikio wa hisia zinazoplekea kufika kileleni zitachelewa hivyo kukuwezesha kudumu katika tendo kwa muda mrefu zaidi na pia itakuondolea hali ya kuweweseka na kuhema ovyo.
 3. Jiachie mnapokuwa faragha
  Inashauriwa kuwa Mwanaume na Mwanamke wanapoingia katika uwanja wa mapenzi wakae kwanza kwa muda, huku wakiwa wamejiachia na mavazi mepesi na ikiwezekana pia wacheze michezo mingi kwa muda mrefu bila kuanza ile “kazi” yenyewe. Hii inaongeza kujiamini na kupunguza uwezekano wa kufika haraka mwisho wa safari.

         > Sababu za kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa

 4. Jibane unapokaribia kumaliza
  Mwanaume anapaswa kujibana akiona dalili za awali za kumaliza bila kujali ametumia muda gani. Anachopaswa kufanya ni kukaza misuli ya miguu na kuzuia mbegu kwa mtindo atumiao kuzuia haja ndogo isitoke. Kujibana huko pia kunatakiwa kuende sambamba na kuacha kucheza “shoo” pamoja na hilo mwanaume anatakiwa aidanganye akili kwa kulazimisha iwaze jambo jingine ili kuharibu taarifa za raha zilizotumwa mwilini zisiendelee kufanyiwa kazi na hatimaye kumfanya kumaliza tendo haraka. Ni vyema ukiona unakaribia mwisho wa safari basi umtoe nyoka pangoni kwa muda ili joto la kwenye shimo liondoke, hii itakuongezea muda zaidi wa kufanya tendo.

Zoezi hili linaweza kuwa gumu katika hatua za kwanza kutokana na kukosea muda sahihi wa kujizuia,lakini mhusika akiendelea kuzoeza atajikuta anaweza na kupata uwezo wa kufanya mapenzi kwa muda mrefu zaidi.

Aidha, kwa wale waliozoea kujichua wanashauriwa kuacha mara moja kwani ni sababu pia ya kufika kileleni mapema, hii ni kwa sababu wanakuwa wamezoea kutumia nguvu sana hivyo wanapokutana na kiungo halisia “UKE” wanashindwa kujizuia kufika kileleni.

error: Content is protected !!