Nabi amtamani Msuva

HomeKitaifa

Nabi amtamani Msuva

Simon Msuva yupo nchini tangu mwaka jana baada ya kuzinguana na timu yake ya Wydad Casablanca ya Morocco na kupelekana Fifa, ila juzi alifunga mabao mawili kwenye mechi ya hisani ya timu Samakiba na kuiwezesha team Kiba kubeba ubingwa wa msimu huu kwa penalti.

Kumbe, kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi alikuwa akimfuatilia dakika zote za mchezo zilizoisha kwa sare ya mabao 3-3, kisha kupigiana penalti na kuweka wazi kuwa kama kuna jina la mchezaji mzawa limesalia kikosi chake ni Msuva anayetamani awe naye.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nabi alisema anatamani kuongeza mshambuliaji mmoja mzawa, lakini kiu ni kuwa na staa huyo aliyewahi kukipiga na kung’ara na Yanga kabla ya kutimkia Difaa El Jadida ya Morocco kisha Wydad.

Nabi alisema anatambua Msuva ana mgogoro na mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, lakini kama mabosi wake wanaosimamia usajili watamfungia kazi wanaweza kunasa saini yake.

“Nahitaji mshambuliaji mwenye kujua kufunga na kasi. Nipo hapa Tanzania kuna wakati ni jambo zuri kuendeleza wachezaji wa taifa hili. Natamani sana kufanya kazi na yule Msuva (Simon),” alisema Nabi.

source: Mwananchi

error: Content is protected !!