Ahadi 6 za Rais Samia kwa wakazi wa Chato

HomeKitaifa

Ahadi 6 za Rais Samia kwa wakazi wa Chato

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amesema Serikali inakamilisha vigezo vitakavyoruhusu Wilaya ya Chato, iliyopo mkaoni Geita, kuwa mkoa.

Rais Samia amesema hayo leo Oktoba 14, 2021 katika kilele cha mbio za Mwenge na kumbukizi ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K Nyerere hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Magufuli na kuongeza kwamba serikali itakamilisha miradi ya maendeleo iliyoachwa na Rais Magufuli wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya kupokea ripoti ya ukaguzi wa miradi mbalimbali iliyowasilishwa kwake na kiongozi wa mbio za Mwenge, Luteni Josephine Mwambashi, Rais Samia amesema bado wilaya hiyo haijawa mkoa na kwamba kama utakidhi vigezo, itakuwa Mkoa.

Aidha, ameahidi kukamilisha ujenzi wa Msikiti mkubwa katika Kata ya Muungano wilayani Chato mkoani Geita, ambao ulianzishwa na Hayati Magufuli kwa kushirikiana na taasisi ya Al-Hikma.

Vilevile Rais Samia ameahidi kutekeleza kwa vitendo ahadi zilizotolewa na Hayati Magufuli kwa watu wa Chato. Ahadi hizo ni pamoja na upanuzi wa Bandari ya Nyamirembe, kukamilisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato, Hospitali ya Kanda Chato, Chuo cha VETA na stendi.

error: Content is protected !!