Wafariki wakidaka kumbikumbi

HomeKitaifa

Wafariki wakidaka kumbikumbi

Watu wawili akiwamo mjamzito, wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika Kata ya Mhembe wilayani Kigoma baada ya kugongwa na pikipiki wakati wanakamata kumbikumbi pembezeno mwa barabara iendayo Gereza la Kwitanga karibu na Mto Kaseke.

Tukio hilo limetokea karibu na eneo la kichungu ambacho wakazi wa eneo hilo hukamata kumbikumbi kila msimu wa masika unapoanza.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Filemon Makungu alisema vifo hivyo vya Neema Moshi (18) na Sia Ramadhan (20) vilisababishwa na dereva anayejulikana kwa jina la Yeovan Kagizo (28) akiwa anaendesha pikipiki yenye namba za usajili MC 602 CPJ kwa mwendo mkali, alishindwa kuimudu na kusababisha ajali iliyosababisha vifo.

Kamanda Makungu alisema Jeshi la Polisi linamshikilia dereva huyo kwa hatua zaidi na kutoa rai kwa madereva bodaboda kuendesha kwa kufuata taratibu na kanuni za usalama barabarani na kuzingatia mwendo unaokubalika kwenye makazi ili wadhibiti pikipiki zao na kuepusha ajali.

error: Content is protected !!