Mafuta ya kula yashuka bei

HomeKitaifa

Mafuta ya kula yashuka bei

Waswahili wanasema baada ya dhiki faraja, hivyo ndivyo tunavyoweza kusema baada ya bei ya mafuta kuanza kushuka kwenye baadhi ya maeneo nchini.

Bei zilianza kupanda hata kabla ya kuanza kwa vita ya Ukraine na Urusi Februari mwaka huu kwa dumu la lita 20 kufikia Sh120,000 hadi Sh130,000 kutoka wastani wa Sh55,000 hadi Sh75,000.

Kwa bei za rejareja lita moja ilifika kati ya Sh8,000 hadi Sh9,000 kutoka Sh5,500 na baadhi ya maeneo yalipanda kutoka Sh6,500.

Godfery James, mfanyabiashara wa duka la rejareja Kinondoni, Dar es Salaam alisema dumu la lita sasa walilokuwa wakinunua kwa Sh115,000 hadi Sh120,000, sasa wanannunua kwa Sh92,000 hadi Sh 94,000.

Alisema lita mota waliyokuwa wakiuza Sh6,500 sasa wanauza Sh 5,500 huku Bryan Wambura, mkazi wa Chanika anayeuza kwa bei ya jumla alisema sasa dumu la lita 20 bei yake ni Sh110,000 hadi Sh100,000 kutoka Sh120,000 hadi Sh130,000.

Jijini Mbeya bei ya mafuta ya kula katika baadhi ya maeneo imeshuka kutoka Sh7,000 mpaka 5,000 na mama lishe kwa sasa wanauza bei ya vyakula imeshuka kutoka Sh2,500 kwa sahani mpaka Sh2,000 na Sh1,500.

 

error: Content is protected !!