Uamuzi wa ombi lao leo

HomeKitaifa

Uamuzi wa ombi lao leo

Mahakama Kuu Masijala Kuu leo inatarajiwa kutoa uamuzi wa ombi la Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee na wenzake 18 endapo wapewe kibali cha kufungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Mdee na wenzake waliwasilisha maombi hayo Mei 13, mwaka huu wakiomba mahakama iwapatie kibali cha kufungua kesi ya mapitio ya kimahakama dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria wa Serikali (CAG).

June 30, mwaka huu maombi hayo yalisikilizwa na Jaji Mustapha Ismail na kupanga kutoa uamuzi le saa 6:00 mchana.

 

error: Content is protected !!