Tanzania yapongezwa mikakati muziri ya uchanjaji

HomeKitaifa

Tanzania yapongezwa mikakati muziri ya uchanjaji

Mratibu wa Kimataifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka umoja wa Mataifa Dkt Ted Chaiban ameipongeza Tanzania kwa kuendeleza mapambano dhidi ya UVIKO-19 na kuweza kuongeza kiwango cha watu waliochanja kutoka asilimia 6.8 hadi kufikia asilimia 12.6 hadi sasa.

Dkt. Ted Chaiban amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuongoza mapambano dhidi ya UVIKO-19, Viongozi wa Wizara pamoja na wadau akiwemo Bi. Zamaradi Mketema kwa kuja na wazo zuri la kuchanja maelfu ya watu katika Maonyesho ya Saba Saba.

“Kuchanja chanjo ya UVIKO-19 kunakupa kinga dhidi ya ugonjwa huo, chanjo inalinda familia yako pamoja na jamii, sisi kama wadau wa maendeleo tuko hapa kusaidia Serikali kuhakikisha inafikia lengo la uchanjaji wa asilimia 70 ili kuwa na Kinga ya Jamii” amesema Dkt. Chaiban.

 

error: Content is protected !!