Chad yapata msamaha wa FIFA

HomeMichezo

Chad yapata msamaha wa FIFA

Baada ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuifungia timu ya taifa ya Chad kutokana na serikali ya nchi hiyo kuingilia ufanyaji kazi wa FIFA kwenye nchi hiyo, marufuku hiyo imefutwa.

Uamuzi umekuja baada ya serikali kurudisha uongozi uliokuwepo na shirikisho hilo kuwa chini ya mamlaka yake yenyewe kama ambavyo FIFA ilitaka.

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Chad amesema kwamba wataanza upya na kufanya vizuri kwa maendeleo ya soka la Chad.

Chad ilitolewa kwenye michuano ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2021 baada ya kufungwa na Sudan 2019.

error: Content is protected !!