Tetesi za Soka Ulaya Leo Oktoba 24 (Suares bado yupo sana Atletico Madrid, Huku Lingard akinyatiwa na Everton, Westham na Newcastle)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya Leo Oktoba 24 (Suares bado yupo sana Atletico Madrid, Huku Lingard akinyatiwa na Everton, Westham na Newcastle)

Klabu ya Everton inaongoza mbio za kumsajili Jesse Lingard (28) kutoka Manchester United lakini kiungo huyo anasakwa pia na vilabu vya West Ham and Newcastle (Football Insider).

Manchester United watafanya kila wawezalo ili kumbakiza kiungo wake, Paul Pogba (28) Old Trafford huku Real Madrid ikiwa na matumaini ya kumsajili nyota huyo kutoka Ufaransa mwisho wa msimu huu (AS – Spanish).

Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Luis Suarez hana mpango wa kuondoka klabuni hapo hata baada ya mkataba wake utakapoisha msimu huu. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 amefunga mabao 5 mpaka sasa msimu huu (Marca – Spanish).

> Tetesi za Soka Ulaya Oktoba 23, 2021

Kocha wa Leicester City, Brendan Rodgers amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kwamba kiungo, Youri Tielemans (25) amekataa kusaini mkataba mpya Leicester City huku nyota huyo akivivutia vilabu kadhaa zikiwemo Liverpool na Manchester United (Mail).

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anamfuatilia kiungo wa Real Madrid Toni Kroos (31) huku mkataba wa sasa wa mjerumani huyo unakwisha mwaka 2023 (El Nacional – Catalan).

Mshambuliaji wa FC Dallas Ricardo Pepi (18) anavivutia vilabu kadhaa vya Ligi kuu England huku Liverpool na Manchester United vikiwa miongoni mwa vilabu vilivyonyesha nia ya kumtaka nyota huyo kutoka Marekani (Mirror).

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Paulo Dybala (27) amefikia muafaka wa kusaini mkataba mpya kusalia Juventus, atasaini mkataba huo muda wowote (Calciomercato – Italian).

Ajax ina nia ya kumbakiza kiungo wake Ryan Gravenberch, ambaye anavivutia vilabu kadhaa vikubwa vikiwemo Liverpool, Manchester United, Barcelona na Juventus, na sasa wanataka kumpa mkataba mpya kinda huyo mwenye miaka 19 (Fichajes – Spanish).

error: Content is protected !!