Wananchi walia kupanda bei ya gesi

HomeKitaifa

Wananchi walia kupanda bei ya gesi

Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wamelia na kulalamikia kuhusu kupanda kwa bei ya gesi ya kupikia nchini tangu Agosti mwaka huu, na  bado sababu ya kupanda kwa bei haijazelezwa huku taarifa zikieleza kwamba huwenda ikapanda zaidi.

Wauzaji na wasambazaji wakubwa wa wa gesi ya Oryx mkoani Kilimanjaro, wamethibitisha kupanda kwa gesi na kueleza hiyo ni kutokana na soko la dunia linavyotaka huku wakihofia gesi hiyo kupanda bei zaidi.

“Tumepewa bei mpya ya gesi, mtungi wa kilo 15 uliokuwa ukiuzwa Sh54,000 sasa utauzwa sh59,000 , mtungi wa kilo sita sasa utauzwa sh25,000.

“Tukiuliza sababu ya kupanda kwa bei tunaambiwa ni kutokana na soko la dunia linavyotaka kwa sababu gesi ni sehemu ya pertoleum, hivyo na sisi kama mawakala lazima tupandishe,” alisema Deoglas Malamsha wakala mkuu usambazaji wa gesi ya Oryx Kilimanjaro.

Mkoa kama Dodoma bado bei ya gesi haijapanda lakini wauzaji wameambiwa watapokea tangazo la kupandisha wakati wowote.

error: Content is protected !!