Mfumo mpya wa maegesho Dar, fahamu jinsi ya kulipia, faida na changamoto zake

HomeKitaifa

Mfumo mpya wa maegesho Dar, fahamu jinsi ya kulipia, faida na changamoto zake

Mkoa wa Dar es Salaam umeanzisha mfumo wa kutoza ushuru wa maegesho kwa njia ya kieletroniki. Mfumo uliokuwa unatumika awali wa risiti za karatasi ambazo hupewa mwenye gari umekoma. Hivi sasa wakusanya ushuru wa TARURA hutumia vifaa maalumu vya kieletroniki ambayo vina ‘scan’ namba ya usajili ya gari ya kuandika deni.

Pamoja na nia njema ya kukusanya mapato kwa maendeleo ya Taifa lakini utaratibu huu una changamoto kadhaa ambazo zinapaswa kufanyiwa kazi ili kupunguza misuguano kati ya mtoza ushuru na mlipa ushuru.

Mtoza ushuru akisha ‘scan’ nambari ya usajili ya gari yako, hakuna taarifa unayopata kama mmiliki wa gari kuwa unadaiwa au una deni la maegesho ni kiasi gani hadi ubonyeze tarakimu namba maalum zilizotolewa na TARURA kutambua deni lako.

     > Njia 3 za kuvutia wateja kwenye biashara yako

Utaratibu huu unaweza kuleta utata kwani mmiliki wa chombo ni ngumu kutambua ni muda gani alipata deni la maegesho, ni tofauti na ule mfumo wa risiti ya karatasi kwani unaweza kujua kwa kuwa kuna kielelezo kinachoonekana. Pili inaweza kuchelewesha mapato kwa Serikali kwani mtu anaweza akalimbikiza deni muda mrefu bila kujua kutokana na ukweli kuwa hakuna alama wala kielelezo kuwa anadaiwa.

Pia ili kuweka imani kubwa kwa wamiliki wa magari/ madereva na kuondoa hisia za kumbakiwa deni na watoza ushuru wa TARURA, ni vyema mashine ikipita ku ‘scan’ gari ya mtu, kuwe na utaratibu wa kupata ujumbe kwa njia ya mtandao unaoonesha muda ambao deni hilo limepatikana pamoja na eneo ambalo deni lilipatikana. Hii itatumika kama kumbukumbun na pia itaondoka utata na kuongeza imani ya watu juu ya TARURA.

Ewe msomaji, pengine hujui au hufahamu kama unadaiwa na TARURA. Ili kujihakikishia kuepuka usumbufu, ni vyema ukatazama kupitia *152*00# na kufuata utaratibu wa namna ya kutazama na kulipa deni lako. Maelezo mengine juu ya kuangalia kama una deni na juu ya kufanya malipo, yameambatanishwa na picha ya tangazo la TARURA lililotoka Tarehe 8 Septemba 2021.

error: Content is protected !!