Fahamu kwanini Facebook, Instagram na Whatsapp zilitoweka hewani

HomeKimataifa

Fahamu kwanini Facebook, Instagram na Whatsapp zilitoweka hewani

Facebook, Instagram na Whatsapp zimerudi tena hewani baada ya kuacha kufanya kazi kwa takribani saa 6 siku ya jana tarehe 4 Oktoba 2021.

Facebook wameeleza kuwa tatizo lililotokea kitaalamu linajulikana kama “Site Down Detector”.

Hili ni jukwaa/mfumo ambao kazi yake kubwa ni kusaidia watu kupokea taarifa kuhusu tovuti mbalimbali na huduma nyingine za kimtandao.

Watumiaji wote wa huduma zinazotolewa na Kampuni ya Facebook wanaotumia kwa njia ya ‘Application’ wezeshi na wale wanaotumia tovuti moja kwa moja, waliathirika na changamoto hiyo.

Facebook wameomba radhi kwa watumiaji wa huduma zake Dunia nzima na kueleleza kwa kina hasa tatizo lilikuwa ni nini?

“Jopo la Wahandisi wetu wamegundua kuwa uchakataji wa taarifa kwenye mtandao wetu mkubwa ambao ndio kama uti wa mgongo wa kuunganisha kati ya facebook na mitandao mingine ndani ya facebook, ilileta shida.

Mkanganyiko huu wa taarifa ulifanya utaratibu wa mawasiliano baina ya vituo vyetu vya taarifa kukwama na kusitisha kabisa taarifa.” Ilieleza taarifa toka Facebook

“Tunajitahidi kurudisha kila kitu kwenye mstari kama kilivyokuwa awali, na tuna imani kwamba changamoto iliyotokea ni changamoto ya kimfumo na hakuna taarifa kwamba tatizo hilo ni udukuzi kutoka nje.”

error: Content is protected !!