Mtoto wa Simbachawene kupanda kizimbani kesho

HomeKimataifa

Mtoto wa Simbachawene kupanda kizimbani kesho

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linatarajia kumfikisha mahakamani kesho mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene, James Simbachawene ambaye kwa sasa yuko nje kwa dhamana.

Kamishna Msaidizi wa Polisi Kanda Maalum, William Mkonda, alisema wamepeleka jalada lake kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwamba likirudi wanatarajia kumpeleka mahakamani Agosti 24, mwaka huu.

“Alikuwa anashikiliwa, lakini ameshaachiwa kwa dhamana kwa sababu ni haki yake ya msingi na tulipeleka jalada leo(jana), lakini halijarudi mapema hivyo tunatarajia kuendelea na taratibu zingine za kumfikisha mahakamani Jumatano,” alisema Mkonda.

error: Content is protected !!