Jaji Mgeta: Waziri Mkuu alichana uamuzi wa Mahakama

HomeKitaifa

Jaji Mgeta: Waziri Mkuu alichana uamuzi wa Mahakama

Jaji mstaafu John Mgeta amesema changamoto iliyomuumiza katika kutekeleza majukumu yake ni kitendo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, kudharau uamuzi wa mahakama kwa kuchana uamuzi aliotoa katia kesi ya mgogoro wa ardhi.

“Kuna changamoto katika mahakama ambayo bado mpaka sasa ipo, serikali kuingilia umamuzi wa mahakama na pia kama serikali ilishatakiwa ikashindwa utekelezaji wa amri ya mahakama unakuwa mgumu.” alisema.

Jaji Mgeta alisahuri mamlaka ya juu iwe inatoa maagizo kwamba maagizo ya mahakama yawe yanatekelezwa.

“Kesi moja niliyoisikiliza nikiwa Arusha, nikatoa uamuzi mwanakijiji aliporwa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa shule. Akataka afidiwe, nikatoa uamuzi ukapelekwa kijijini kwa ajili ya utekelezaji lakini alikuwepo mkuu mmoja, akiwa likizo huko kijijini alichana ule uamuzi.

“Aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo simkumbuki , alikuwa anatokea Monduli. Aliniumiza sana kuona kwamba mahakama haikuthaminiwa. Shule iliendelea kujengwa lakini baadaye yule mwanakijiji alifidiwa baada ya mahakama kudharauliuwa,” alisema Jaji Mgeta.

Jaji Mgeta alitoa aliyasema hayo jana Mahakama Kuu Masijala Kuu Dar es Salaam katika hafla ya kitaaluma ya kuwaaga majaji wastaafu, Jaji Mgeta, Jaji Beatrice Mutungi na Jaji Sekela Moshi.

 

error: Content is protected !!