Ruksa mabasi kuanza safari saa tisa usiku

HomeKitaifa

Ruksa mabasi kuanza safari saa tisa usiku

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeruhusu mabasi ya mikoani yaanze safari saa tisa usiku.

Latra imeagiza wamiliki wa mabasi wanaopenda kuanza safari muda huo wafike katika ofisi za mamlaka hiyo kuomba leseni na masharti ni lazima madereva wasajiliwe ili kuwa na taarifa zao.

Priscus Joseph, Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) alisema hayo jana Dar es Salaam akiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Latra, Salum Pazzy.

Pazzy alisema kuwa Latra inafanya kazi kwa kushirikiana na wadau wakiwamo Taboa na hawana mvutano kuhusu muda wa kuanza safari za mabasi kwenda mikoani.

error: Content is protected !!