Mwigulu kusomesha watoto wa diwani aliyekufa ajalini

HomeKitaifa

Mwigulu kusomesha watoto wa diwani aliyekufa ajalini

Mbunge wa Singida Magharibi, Dk Mwigulu Nchemba ameahidi kulipa ada za masomo ya watoto wa aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Kinampanda wilayani Iramba, Winjuka Mkumbo aliyekufa kwenye ajali ya gari wilayani Manyoni mkoani Singida.

Dk Mwigulu ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango, alitoa ahadi hiyo wakati wa mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Kijiji cha Simbalugwala, Kata ya Mukulu wilayani Iramba mkoani Singida.

Alisema kifo cha Winjuka kimemsikitisha kwa kuwa licha ya utendaji kazi wake, alikuwa rafiki wa karibu wa familia yake.

“Naahidi kugharamia ada za watoto wa marehemu ambao wapo katika ngazi mbalimbali za elimu ili waweze kutimiza ndoto zao,” alisema Dk. Mwigulu.

Alisema Winjuka alipenda maendeleo ya wananchi na nchi yake na alihubiri umoja, upendo na mshikamano.

error: Content is protected !!