Walimu waliomcheka mtoto akichapwa wasimamishwa kazi

HomeKitaifa

Walimu waliomcheka mtoto akichapwa wasimamishwa kazi

Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Toba Nguvila amewasimamisha kazi watumishi watano akiwamo Mratibu Elimu Kata ya Kalanja na walimu wanne waliokuwa wanacheka wakati mwalimu Isaya Emmanuel akiwaadhibu watoto kwa fimbo.

Nguvila ameamua hivyo kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila aliyeagiza watumishi hao wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu.

Waliosimamishwa kazi ni Mratibu wa Elimu Kata ya Kalanja, Sweatbert Kiiza na walimu, Godson Rwabisho, Beatrice Kaburanyange, James Josiah na Delpina Leonce.

Pia walimu watatu kati ya hao wamehamishwa kituo cha kazi na wamepewa barua ya onyo.

error: Content is protected !!