Rais Samia atoa maelezo kuhusu wanafunzi waliojifungua kuendelea na masomo

HomeKitaifa

Rais Samia atoa maelezo kuhusu wanafunzi waliojifungua kuendelea na masomo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu ametilia mkazo agizo la Waziri wa Elimu, Joyce Ndalichako kwamba wanafunzi wote waliopata ujauzito na mambo megine yaliyowafanya wasiendelee na masomo, sasa wameruhusiwq kurudi shule.

“Tumeamua watoto wote walioacha shule kwa sababu mbalimbali: utoro, sababu za kisheria kwamba ukipata mimba hauruhusiwi kuendelea na masomo, lakini wale waliodondoka la saba (tunajua tuna wanafunzi wetu wazuri sana kwa bahati mbaya wakati wa mtihani ni mtihani hawakufanya vizuri) lakini baada ya kukaa nje nakujutia tunawapa nafasi nyingine yakufanya mitihani,” amesema Rais Samia.

Aidha , Rais Samia amesema lengo la maamuzi hayo ni kutoa fursa pana kwa watoto Wakitanzania kuweza kuendelea na elimu huku akieleza njia mbadara kwa wale watakaoshindwa kuendelea na masomo Serikali imeenda mpango mbadara wakuwafanya watoto hao kuendeleza ndoto zao.

error: Content is protected !!