Muhtasari wa kitabu alichoshika Mbowe mahakamani leo

HomeMakala

Muhtasari wa kitabu alichoshika Mbowe mahakamani leo

Leo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe alionekana akiwa ameshika kitabu ndani ya Mahakama. Kitabu alichoshika Mbowe kina picha ya Malcolm X (mwanaharakati wa Marekani aliyekuwa akipigani haki za watu weusi kabla kuuwawa mwaka 1965) na jina ‘The Dead Are Arising”

Tumekuandikia ufupisho wa kitabu hicho kilichoandikwa na mwandishi kutoka nchini Marekani, Tamara Payne ameandika kitabu hicho kilichoangazia wasifu wa Malcom X

Tamara Payne ni mtoto wa mwandishi Leslie Payne (alifariki mwaka 2018) ambaye alifanya utafiti wa muda mrefu kwa kuaznia mwaka 1990. Leslie Payne aliwahoji watu wengine ambao walijuana kwa ukaribu kabisa na Malcolm X (ndugu zake, watu aliosoma nao, marafiki zake, wanaharakati wenzake, wapelelezi (FBI) na viongozi wa kisiasa). Lengo lake ilikuwa kupata mahojiano halisi ambayo yangeweza kuelezea vizuri maisha ya Malcolm X.

Matokeo ya utafiti huo wa muda mrefu, yalisaidia kupatikana kwa kitabu cha ‘The Deas are Rising’ ambapo jina la kitabu hicho linatokana na maneno ambayo Malcolm X aliwahi kuwaambia wafuasi wake (Wafu wanasimama tena/wanafufuka) alipokuwa akiwapa moyo na kuwahamasisha katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi. Kitabu kinaelezea maisha ya Malcolm X kama ‘mhalifu wa mtaani aliyekuja kuwa mwanamapinduzi wa kuaminika’

>Mfahamu Freeman Mbowe: CHADEMA, Benki Kuu, biashara na kesi ya ugaidi

Tamara Payne ambaye pia alikuwa mtafiti wa Baba yake (Leslie Payne), alikamilisha vyema kazi ya baba yake kwa kaundika kitabu hicho. Kitabu kinaeleza maisha ya Malcolm X tangu kuazaliwa kwake huko Nebraska Marekani mwaka 1925 hadi kuuwawa kwake mwaka 1965. Kinaeleza ushawishi wa wazazi wake katika kumfanya awe mwanaharakati. Kila sura ya kitabu hicho imepambwa na na visa na matukio ya kweli yanayomhusu Malcolm X.

Kitabu hicho pia kinaeleza kwa undani kuhusu hatua za Malcolm X kwenye harakati zake, washirika wake kwenye mapambano hadi namna alivyokutana na kundi lililomuua (KKK).

Freeman Mbowe alionekana akitabasamu huku akionesha kitabuy hicho leo hii wakaati wa kusikilizwa kwa kesi ya ugaidi inayomkabili yeye na wenzake watatu. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kesho (Novemba 3)

error: Content is protected !!