Bajeti ya Zanzibar raha

HomeKitaifa

Bajeti ya Zanzibar raha

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) jana imewasilisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka 2022/23 ya Sh2.5 trilioni huku ikitarajia kuanza kuwalipa mishahara madiwani wadi ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Akisoma hotuba ya bajeti hiyo kwa Baraza la Wawakilishi jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya alisema kati ya Sh2.5 wanazotarajia kukusanya, mapato ya ndani ni Sh1.3 bilioni, misaada na mikopo kutoka kwa washirika wa maendeleo ni Sh687.95 bilioni, mikopo ya ndani na nje kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ni Sh515.0 bilioni.

Waziri Mkuya alisema Sh trilioni 1.3 ikiwa sawa na asilimia 53 ni kwa ajili ya matumizi ya ndani na kutekeleza miradi ya kimkakati na Sh trilioni 1.2 zimetengwa kwa kazi za kawaida . Sh bilioni 17.60 zitatumika kwa ajili ya serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na kuwalipa madiwani.

Aidha, alitaja marekebisho yaliyofanyiwa kazi ni pamoja na sheria ya ushuru wa hoteli namba 1 ya mwaka 1995 pamoja na kupunguza kiwango cha ushuru wa forodha ili kushajihisha uwekezaji katika uzalishaji wa viwanda vya nguo.

 

error: Content is protected !!