Amuua rafiki yake baada ya kumnyima pombe

HomeKimataifa

Amuua rafiki yake baada ya kumnyima pombe

Polisi Kaunti ya Kirinyanga nchini Kenya, inamshikilia mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Wycliff Kinyua (26) kwa tuhuma za kumuua rafiki yake Alex Maina (30) baada ya kumkumnyima pombe.

Wawili hao wanajihusisha na uendeshaji wa pikipiki (bodaboda) walipewa ofa na rafiki yao mmoja ya kuwanunulia bia na ndipo ugomvi ulipoanza baada ya Alex kumnyima Wycliff pombe.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Ndia, David Kabena alisema Kinyua amekamatwa na kuhifadhiwa katika kituo cha Polisi cha Sagana wakati upepelezi ukiendelea.

 

error: Content is protected !!