Bashungwa apigwa spana na Samia

HomeKitaifa

Bashungwa apigwa spana na Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Ripoti ya TAKUKURU leo tarehe 30 Machi, 2022 Ikulu Chamwino, Dodoma amemtaka Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa kufuatilia wastaafu na waliofariki ambao bado wanaonekana wakipokea mishahara.

“Bado kuna watu walishafariki na kustaafu lakini bado wanaonekana kwenye orodha ya waopokea mishahara, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Inno chukua hatua pale unapoona kuna ushahidi , wanasema mchelea mwana kulia, hulia mwenyewe,” alisema Rais Samia Suluhu.

Aidha, Rais Samia pia alieleza sababu ya kupanda kwa bei ya mafuta nchi baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi.

“Wabunge wenye maeneo yenu, mawaziri mnaosimamia sekta waambieni wananchi ukweli, vita ya Russia na Ukraine imepandisha sana bei ya mafuta na mafuta yanapopanda ndio kila kitu kinapanda,” alisema Rais Samia Suluhu.  

error: Content is protected !!