Juhudi za Rais Samia kufanikisha mradi wa gesi asilia nchini

HomeKitaifa

Juhudi za Rais Samia kufanikisha mradi wa gesi asilia nchini

Na George Bura, Dar es Salaam

Juni 11, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya awali na kampuni kubwa za uchimbaji mafuta duniani zikiwemo Equinor na Shell kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa uchakataji na usimikaji gesi asilia (LNG) wenye thamani ya Dola za Marekani 30 bilioni sawa na Sh70 trilioni.

Utiaji saini wa mkataba wa nchi hodhi (HGA) yamefikia ikiwa ni zaidi ya miezi sita tangu serikali ya Awamu ya 6 irejee tena majadiliano na wawekezaji hao Novemba mwaka jana baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kueleza kuwa anataka kuona mradi huo ukiendelea kwa manufaa ya Watanzania.

“Utakapokamilika mradi huu utabadilisha taswira ya uchumi wa nchi yetu. Natazamia kukamilika kwa majadiliano Desemba (mwaka huu) na mradi huu uanze,” alisema Rais Samia akiagiza kipaumbele kitolewe kwa makandarasi wa ndani na kuwataka wajiandae kwa fursa hizo.

Mkuu wa Nchi alibainisha kwamba, Watanzania watanufaika sana kutokana mradi huo kwani unatarajia kutoa ajira 10,000 kwa wakati wa ujenzi wake ambapo zitapungua hadi 500 utakapoanza kufanya kazi huku ukitajwa kuwa na manufaa makubwa kiuchumi kwa sababu utaongeza uhakika wa nishati na kuipatia nchi fedha za kigeni.

Endapo mradi huu utakamilika, gesi itaanza kutumika kwenye nyumba na kwenye huduma za kijamii na maboresho makubwa yatafanyika kwa Uwanja wa Ndege wa Mtwara, barabara na huduma za kijamii kwa kuwa shule, vituo vya afya vizuri, maji na
umeme.

error: Content is protected !!