Mdee na wenzake watuma barua kwa spika

HomeKitaifa

Mdee na wenzake watuma barua kwa spika

Wabunge 19 wa viti maalumu waliofutiwa uanachama CHADEMA, wamewasilisha tena maombi namba 27/2022 ya kuomba kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama katika Mahakama Kuu Masjala Kuu, Dar es Salaam.

Vilevile, wabunge hao wamewasilisha maombi madogo namba 16/2022 ya kuiomba mahakama kutoa zuio la muda kutochukuliwa hatua yoyote ikiwamo wabunge hao kubaki na hadhi yao hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Wamefikia hatua hiyo baada ya kufanya marekebisho waliyoambiwa wayafanye katika maombi ya awali yaliyotupwa Juni 22,2022 na Jaji Mfawidhi John Mgeta.

Aidha, tayari wabunge hao wameshamwandikia Spika wa Bunge kumfahamisha kwamba wameshawasilisha kesi mpya mahakamani.

error: Content is protected !!