Ujumbe wa RC Makalla kwa Mwijaku na Baba Levo

HomeKitaifa

Ujumbe wa RC Makalla kwa Mwijaku na Baba Levo

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Amos Makalla amewataka akina Baba Levo na Mwijaku kuanza kuhamasisha watu kwenye kufanya usafi na kutunza mazingira baina ya timu zao badala yakuchochea ‘bifu’ (ugomvi) baina ya wasanii aua watu maarufu nchini.

“Kwahiyo akina Mwijaku akina Baba Levo na wengine wote nataka debe kubwa kwenye usafi sasa, wanaongea sana na wazuri sana kwenye kuongea sasa nataka hiyo. Wale wasemaji wale na najua mabalozi wanatimu zao basi sasa hivi akili yote iwe kwenye usafi, twendeni huko itatusaidia sana,” amesema Makalla.

RC Makalla amesema hayo akiwa anazindua mpango wa usafi wa Dar es Salaam huku mabalozi wa mazingira kama msanii Ali Kiba na Harmonize wakihudhuria uzinduzi huo.
Mheshimiwa. Makalla amewataka wasanii na watu maarufu kuhamasisha wananchi kufanya usafi

error: Content is protected !!