Tozo yawaliza Hanscana, Lavalava na Mbosso

HomeBurudani

Tozo yawaliza Hanscana, Lavalava na Mbosso

Mtayarishaji wa video nchini Hanscana amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuhusu changamoto za tozo kubwa wanazokutana zao pindi wakitaka kufanya kazi kwenye vivutio vya kitalii na kusema kuwa gharama zilizowekwa ni kubwa mno ikizingatiwa wao ni wazawa sio wageni.

Baada ya kuandika hivyo wasanii wengine kutoka lebo ya Wasafi, LavaLava na Mbosso nao pia wakafunguka na kusema huwa wanakutana na changamoto hizo za gharama kubwa au kulazimika kuandika barua ambayo huchukua takribani mwezi kujibiwa hivyo kukwamisha kukamilisha kazi zao za kisanii kwa wakati.

Katika malalamiko hayo Hanscana ameomba baadhi ya viongozi wa serikali kuingilia kati suala hili huku akimtaja Mbunge wa Morogoro Kusini Mshariki, Hamisi Tale na Mbunge wa Muheza Hamisi Mwinjuma kuwasaidia.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by GODFATH3R (@hanscana_)

error: Content is protected !!