Adele kuachia albamu  inayoelezea ndoa yake iliyovunjika

HomeBurudani

Adele kuachia albamu  inayoelezea ndoa yake iliyovunjika

Staa wa muziki toka nchini Uingereza, Adele amesema anatarajia kutoa albamu ambayo itakua maalum kwa ajili ya mtoto wake wa miaka 9. Akizungumza na jarida la Vogue, Adele amesema kwamba anataka mtoto wake ajue kwanini yeye na baba yake waliachana.

Adele amefafanua kuwa kuachana kwake na Baba wa mtoto wake ni kitu kinachosababisha muda mwingine mtoto huyo akose raha. Ameenda mbali zaidi akisema kuwa hali hiyo ni kidonda kwake ambacho hajui atakitibu vipi lakini anataka mtoto wake akifikia umri wa miaka ya 20 hadi 30 ajue yeye (Adele) ni nani na kwanini aliacha yote ili kutafuta furaha.

Albamu hiyo ambayo itakua ya nne kutoka kwa Adele imepewa jina la ‘30’ ambao ni umri ambao Adele aliolewa na mwanaume huyo aliyemuacha.

error: Content is protected !!