Wanawake wenye miguu ya thamani zaidi duniani

HomeBurudani

Wanawake wenye miguu ya thamani zaidi duniani

Wakati sehemu kubwa katika jamii zetu wakishindwa kumudu gharama za kukata bima kwa ajili ya afya na mali zao kama magari, nyumba, ofisi na viwanja, unaweza kushangazwa na watu maarufu ambao wameamua kukata bima kwa ajili ya  miguu tena kwa mamilioni ya fedha.

Kwa mujibu wa tovuti ya Fox Business bima ya sehemu ya mwili au viungo hukatwa ili kufidia gharama za matibabu kwa mtu ambaye miguu yake itapata changamoto yoyote ikiwemo ajali, ulemavu na hata makovu.

Ifuatayo ni kati ya miguu ya Wanawake  ambayo thamani ya bima yake huenda ikakujengea nyumba na hata kukufanya uuage umaskini.

1. Mariah Carey
Miguu ya mwanamke huyu mwenye sauti inayokosha wengi akiwepo stejini ilikatiwa bima yenye thamani ya dola za Kimarekani, bilioni 1 sawa na shilingi za Kitanzania trilioni 2.3 trilioni. Mwaka 2006 Gillette Venus, kampuni inayotengeneza nyembe za kunyolea ilimtunuku Mariah Carey  tuzo ya miguu bora nchini Marekani.

2. Taylor Swift
Mwaka 2015, Swift akiwa kwenye ziara ya kimuziki iliyojulikana kama “1984”, aliikatia bima miguu yake kwa thamani ya dola za Kimarekani milioni 40 (Sawa na takribani shilingi bilioni 92.8). Alifanya hivi ili kuhakikisha show zake zinakamilika hata pale atakapopata shida yoyote.

3. Tina Turner
Turner (81) amewahi kuikatia miguu yake bima yenye thamani ya dola za Kimarekani 3.2 milioni (Sawa na shilingi za Kitanzania 7.4 bilioni) na mwaka 1994 alitunga wimbo wa “Legs” kwa ajili ya kudadavua kazi ya miguu yake.

4. Heidi Klum
Huyu ni miongoni mwa majaji wa muda mrefu kwenye mashindano ya kusaka vipaji nchini Marekani, “America’s Got Talent” akiwa na nguli wengine kama Mel B kutoka Spice Girls na Simon Cowell.

Miguu ya Klum iliwahi kukatiwa bima yenye thamani ya Dola za Marekani 2 milioni (Sawa na shilingi za Kitanzania 4.6 bilioni) kuhakikisha kuwa ipo salama wakati wote hata akitembea kwenye viatu virefu kwenye majukwaa mbalimbali.

Unaweza Ukastaajabu hayo lakini wapo watu wengine maarufu ambao wameweka bima kwenye mambo kama vile ndevu, makalio na hata uso.

error: Content is protected !!