Makosa ambayo Mwanaume utakiwi kufanya kwenye muonekano wako

HomeElimu

Makosa ambayo Mwanaume utakiwi kufanya kwenye muonekano wako

Mara nyingi watu wanavaa ili wapendeze bila kujali anavaaje, wakati gani na muda gani. Kwenye kuhakikisha unakua na muonekano mzuri unapotoka ni lazima uzingatie kanuni za uvaaji. Kuna makosa watu hufanya kwenye mitindo ambayo huweza kuonekana kawaida ila hutakiwi kabisa kujaribu kuyafanya. Makosa hayo ni pamoja na:

1. Kuvaa nguo ambayo haijanyooshwa
Wapo ambao wanavaa nguo zenye mikunjo lakini wakiulizwa wanasema wamenyoosha, nguo kama hizo zinakua na kitambaa kigumu hivyo unatakiwa kuzingatia wakati wa kunyoosha lakini pia unapoanua kwenye kamba zikunje usizitupie wala kurundika. Nguo iliyoonyoshwa inakufanya uonekane nadhifu

2. Usivae soksi za mazoezini kama huendi mazoezini
Mara nyingi hii hutokea kwa Wanaume na unaweza kukuta Kaka mtanashati amevaa vizuri anaenda kazini ila kavaa soksi za kuendea mazoezini. Unachotakiwa kujua soksi za kazini au mtoko ni zile zenye rangi iliyopoa zilizotengenezwa kwa hariri au pamba kwa kiasi kikubwa na cha muhimu ni kwamba hutakiwi kuvaa soksi nyeupe.

3. Fungua vifungo vya koti unapokaa
Ikitokea umevaa koti la suti kama lina kifungo kimoja kifungue unapokua umekaa na kifunge unaponyanyuka. Kama koti lina vifungo viwili funga kifungo cha juu tu unaponyanyuka na kama ni la vifungo vitatu funga vifungo viwili vya juu. Hii itakufanya suti yako isijikunye pia utaonekana kuwa mtu makini.

4. Usivae viatu vichafu
Hata upendeze vipi kama viatu vyako ni vichafu basi utakuwa umefanya  kazi bure tu,  kwani vitaharibu muonekano wako wote na hutokosa kutolewa kasoro. Sasa unachotakiwa ni kuhakikisha viatu vyako ni visafi muda wote.

Kwa kuzingatia hayo unaweza pia kuongeza vivalio kama cheni, saa bila kusahau kunyunyiza ‘perfume’ kwa ajili ya kunukia vizuri.

error: Content is protected !!