Vyakula Kumi (10) vinavyoongeza hamu ya tendo la ndoa

HomeElimu

Vyakula Kumi (10) vinavyoongeza hamu ya tendo la ndoa

Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kunaweza kutokea kutokana sababu kadhaa ikiwemo uzalishwaji mdogo wa homoni ya testesterone, matumizi ya dawa, kufanya sana mazoezi au kutofanya kabisa, unywaji wa pombe lakini pia matumizi ya dawa za kulevya vinaweza kuchochea kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Pia msongo wa mawazo, sonona pamoja na mkazo ni sababu. Hali ya kukosa hamu ya kuvinjari katika tendo la kujamiina imeleta na inaendela kuleta taharuki nyingi katika ndoa na mahusiano ya watu wengi.

Hupaswi kuwa na wasiwasi sana pindi hali hii inapokukuta, unaweza kuanza kutumia vyakula ambavyo vimethibitishwa kisayansi ambavyo vinaweza kuondoa au kupunguza tatizo hilo. Vyakula hivyo ni kama ifuatavyo.

1. Pilipili.
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinaitwa Capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali. Capsaicin huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo huleta mguso wa hisia za raha wakati wa kufanya tendo la ndoa. Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kuamshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati wa tendo la ndoa na pia ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa unapata hisia kila sehemu ya mwili.

2. Matunda na mboga za majani.
Ulaji wa matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol). Kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu. Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha uwiano wa uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homon za testosterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na pia kupelekea mwanaume kuwa na hisia finyu za mapenzi. Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia au kuwa na hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua. Kitalaam inashauriwa kula milo 3 ya matunda kwa siku.

3. Nafaka zisizokobolewa.
Nafaka hasa zisizokobolewa kama mahindi, ngano, uwele, nk zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu. Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo. Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya njema na mahusiano mazuri ya ndoa yako.

4. Tangawizi.
Tangawizi ni kiungo cha mboga ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume hivyo kuwa na umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza kuliwa mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula au kusagwa na kuwa kama unga na kutumiwa kama chai.

5. Asali.
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke. Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.

> Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

6.  Karanga.
Karanga huhusika katika kuchochea mfumo wa mzunguko wa damu (vascular system). Mzunguko wa damu ulio sawasawa katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa murua. Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za mwanaume.

7. Chaza (Oysters) na pweza.
Hawa ni aina ya samaki ambao hupatikana katika maji chumvi. Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume. Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume. Pia madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa kwa wanaume.

8. Soya.
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha mafuta (fat) na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause(kukoma kwanhedhi) kutengeneza homoni estrogen ya ziada. Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimuliwa wakati wa tendo la ndoa.

9. Chocolate.
Chocolate ina Phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni (orgasm). Inasaidia sana kula chocolate masaa machache kabla ya kuanza kufanya tendo la ndoa.

10. Parachichi.
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa Wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiana.

error: Content is protected !!