Matukio aliyowahi kufanya Kizz Daniel

HomeBurudani

Matukio aliyowahi kufanya Kizz Daniel

Juni 2022: Alizua hasira nchini Zambia, nusura show yake izuiwe kufuatia dharau kwa waandishi wa habari na kumsukuma shabiki yake mmoja aliyejaribu kumpa Maua wakati akiwasili Uwanja wa Ndege.

Julai 2022: Alizomewa na Mashabiki Maryland nchini Marekani baada ya kuchelewa kwa masaa manne na kusababisha kutupiwa vitu wakati akitumbuiza jukwaani.

Julai 2022: Aliwakasirisha mashabiki wa Denver nchini marekani baada ya kuifuta show yake ambayo alitakiwa kuifanya na kupelekea mashabiki kutumia mitandao ya kijamii kumshambulia

August 2022: Aliwasilia Tanzania saa chache kabla ya Show huku akishindwa kutumbuiza kwa sababu mbalimbali ikiwemo begi lenye mavazi kusahaulika Airport alikotoka.

error: Content is protected !!