Kaoneka: aliyepigwa anakuwa tajiri, mimi najisikiaje?

HomeBurudani

Kaoneka: aliyepigwa anakuwa tajiri, mimi najisikiaje?

Mwanamasumbwi Shabani Kaoneka amesikitishwa na kitendo cha Karim Mandonga kupewa nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari na kupata madili ya matangazo mbalimbali ilihali yeye alishinda pambano katika ya wawili hao.

“Mbona Mandonga mnamuita, mimi niliyeshinda nakuwa masikini aliyepigwa anakuwa tajiri mimi najisikiaje,” amesema Kaoneka.

Mandonga  amekua akionekana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii akihojiwa na pia kupewa ubalozi wa bidhaa mbalimbali kutoka katika kampuni tofauti licha ya yeye kupigwa kwenye mtanange kati yake na Kaoneka.

error: Content is protected !!