Royal Tour Tanzania yazidi kujibu

HomeKitaifa

Royal Tour Tanzania yazidi kujibu

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imepokea meli nyingine iliyobeba watalii kutoka Ufaransa.

Meli hiyo ya utalii ijulikanayo kam LE JACQUES – CARTIER PONANT ilifika jana ikiwa imebeba watalii 125 ambao wametembelea Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia, Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kwa ajili ya kufanya utalii wa malikane na fukwe.

Meli hiyo inaendelea na safari katika visiwa vya Pemba na Unguja.

Juzi Mkuu wa KItengo cha Uhusiano wa Umma wa TAWA, Vicky Kamata alisema meli hiyo ni ya pili kuja nchini ndani ya wiki hii baada ya nyingine , Corals Geographic Cruise ya Australia kutia nanga ikiwa na watalii 120.

Ujio wa watalii hao ni matunda yatokanayo na filamu ya (The Royal Tour) ilichezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

error: Content is protected !!