Maboresho Bandari ya Tanga yamkosha Balozi wa Rwanda nchini

HomeKitaifa

Maboresho Bandari ya Tanga yamkosha Balozi wa Rwanda nchini

Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba amefanya ziara ya kutembelea Bandari ya Tanga.

Lengo la ziara hiyo pamoja na mambo mengine ni kuona maendeleo ya mradi mkubwa wa kimkakati wa maboresho ya Bandari ya Tanga ambao kwa sasa umefikia asilimia 95 ya utekelezaji wake.

Balozi Karamba amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan za kuboresha Bandari ya Tanga na kuelezea utayari wa Nchi ya Rwanda kutumia Bandari hiyo kupitisha Shehena zake.

 

error: Content is protected !!