Waziri Makamba asisitiza matumizi ya nishati safi kwa maendeleo

HomeKitaifa

Waziri Makamba asisitiza matumizi ya nishati safi kwa maendeleo

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema tarehe 1 na 2 mwezi Novemba mwaka huu kutakuwa na Kongamano la Kuongeza Matumizi ya Nishati Safi na Salama nchini litakalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatajariwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, Waziri Makamba alitaja dhamira ya Kongamano hilo kuwa ni kufahamu hali ya sasa ya nishati ya kupikia ilivyo nchini, kubadilishana uzoefu na ujuzi na fursa zitakazoweza kuondokana na kutatua changamoto za upanitakanaji wa nishati safi ya kupikia.

Pia, kupitia na kijadili sera, sheria pamoja na mikakati ya kifedha na kieletroniki itakayowezesha kuelekea kwenye nishati safi na salama, kongamano hilo litasaidia kutafuta namna bora ya kufikia malengo hayo na kutengeneza ushirika na ushirikiano na maelewano miongoni mwa wadau.

Aidha, Waziri Makamba amesisitiza kuongeza matumizi ya nishati safi na salama nchini ili kuepukana na maradhi yanayotokana na upumuaji wa moshi kwani itaipunguzia mzigo sekta ya afya, itaboresha maisha ya Watanzania kiafya, kiuchumi na kijamii , lakini pia itawezesha ustawi wa wanawake na ushiriki wa wao kwenye shughuli za maendeleo kwa ukamilifu.

 

 

 

 

error: Content is protected !!