Menina awashtaki DSTV, Juma Lokole na Maimartha, ataka kulipwa bilioni 1.1

HomeBurudani

Menina awashtaki DSTV, Juma Lokole na Maimartha, ataka kulipwa bilioni 1.1

Mwanadada, Menina Abdulkarim Atiki ambaye ni mwimbaji, mwigizaji na mshereheshaji ameishtaki kampuni ya Multichoice toka Afrika Kusini (wamiliki wa DSTV) ambayo kwa Tanzania inajulikana kama Multichoice Tanzania, kwa kurusha maudhui yaliyomchafua na kusababisha uharibifu wenye thamani ya bilioni 1.1.

Katika kesi hiyo ya namba 133 ya 2021 Washtakiwa wengine ni Mhariri wa ICU- Chumba cha Umbea kinachoruka kwenye kituo cha Maisha Magic Bongo kwenye DSTV, Watangazaji wa kipindi hicho ambao ni Maimartha Jesse, Juma Lokole na Kwisa Thompson (Kamanda Mzee Mkavu).

> Alikiba afunguka kuhusu kuimba ‘Amapiano’

Mlalamikaji, Menina anasema aliharibiwa kiakili na kihisia baada ya watangazaji hao kwenda kwenye msiba wa mume wake na kuwahoji majirani na ndugu wa mumewe na kumshutumu yeye kuwa alikuwa mke ambaye hakumuhudumia mumewe wakati wa ugonjwa huku wakitaja kama mke asiyewajibika.

Menina anasema itamchukua karibu mwaka kusafisha jina lake ambalo limeharibiwa, kesi hiyo ilisikilizwa kwa mara ya kwanza Septemba 27 lakini kampuni ya Multichoice Tanzania hawakuwepo hivyo kesi ilihairishwa mpaka Novemba 10, 2021.

error: Content is protected !!