Alikiba afunguka kuhusu kuimba ‘Amapiano’

HomeBurudani

Alikiba afunguka kuhusu kuimba ‘Amapiano’

Mfalme wa Bongo fleva anayetamba na albamu ya ‘Only One King’ aliyoizindua hivi karibuni, Alikiba amesema kwamba sio lazima aimbe mtindo wa Amapiano kwa kuwa kuna mitindo mingi ya kuimba.

Alikiba amefunguka hayo kutokana na watu wengi kutegemea pengine kungekuwa na uwepo wa wimbo wenye mahadhi ya Amapiano katika albamu yake kwani, kwa sasa wasanii wengi wamekuwa wakiimba nyimbo hizo hasa pale wafanyapo kazi na wasanii kutoka Afrika Kusini.

 > Uchambuzi mfupi wa album mpya ya Alikiba (Only One King)

“Kama wao wanafanya waache wafanye, lakini sio kila unapofanya kazi na mwanamuziki wa Afrika Kusini lazima uimbe Amapiano.” alisema King Kiba.

Ikumbukwe wimbo namba 12 kwenye albamu hiyo unaokwenda kwa jina la Niteke amewashirikisha Blaq Diamond kundi la wasanii kutoka Afrika Kusini lakini hajatumia mtindo wa Amapiano kwenye wimbo huo.

error: Content is protected !!