Zingatia haya kabla ya kununua akaunti ya Twitter

HomeElimu

Zingatia haya kabla ya kununua akaunti ya Twitter

Biashara ya kuuza na kununua akaunti za mitandao inazidi kukua siku baada ya siku. Moja kati ya ‘akaunti’ zilizo katika uhitaji (demand) mkubwa kwa sasa ni za mtandao wa Twitter hasa ukizingatia kuwa ni ngumu sana kukuza akaunti ya Twitter ukilinganisha na akaunti za mitandao mingine.

Wengi hununua akaunti kwa kigezo cha kuwa na wafuasi wengi, lakini ukweli ni kwamba hilo ni kosa kubwa sana kwa hicho hakipaswi kuwa kigezo pekee cha kumfanya mtu anunue akaunti na wengi wameshapata hasara kwa kutumi kigezo hicho pekee. Hapa swali linabaki, je, ni vigezo gani vingine unaweza kuvitumia kabla ya kununua akaunti ya Twitter? Tumeviweka vigezo vyote hapa

  1. Analytics
    Kama ni mtumiaji wa Twitter, basi omba analytics za akaunti unayotaka kununua, na kama huna uelewa wa hili ni vyema ukatafuta mjuvi wa mtandao wa Twitter akupe ushauri na kukusaidia kuelewa kilichomo katika ‘analytics’ kabla ya kuamua kununua akauti husika.
    Ukifunga kipengele cha analytics, utakutana na vitu vitatu muhimu, ‘Impressions’, ‘profile visits’ na ‘mentions’.

(a) Impressions
Impression inatumika kuonesha ni mara ngapi watu wamekutana na tweets za akaunti hiyo. Hawa ni wale watu ambao wameiona tu tweet hiyo, bali kucomment, kulike wala kufanya chochote. Twitter wana utaratibu wa kuonesha tweets zako zimeonekana mara ngapi ndani ya siku saba, siku 28 hata miezi ya nyuma. Takwimu hii ni kigezo muhimu sana kujua akaunti inaweza kufikia watu wangapi kama utaweka tangazo au taarifa fulani. Kuwa na wafuasi wengi bado sio kigezo cha akaunti kuonekana mara nyingi zaidi, akaunti inaweza kuwa na wafuasi kidogo, lakini inaonekana na watu wengi kutokana na aina ya maudhui yanayochapishwa.

(b) Profile Visits
Hii kazi yake ni kukuonesha ni watu wangapi wamepekua akaunti yako, kuitazama kutaka kukujua zaidi. Idadi ikiwa kubwa zaidi maana yake ni kwamba watu wanakufuatilia zaidi, na ikiwa ndogo ni kwamba watu hawavutiwi kutazama au kukujua zaidi labda kutokana na aina ya maudhui.

> Njia 7 rahisi za kukuza akaunti yako ya Twitter kutoka ‘follower’ 0-1000 ndani ya mwezi mmoja

(c) Mentions
Mention ni jina unalotumia kuhusishwa kwenye mijadala ya Twitter. Hii ni hatua ambayo itaonesha ni namna gani akaunti ni kubwa au ndogo. Akaunti kubwa na maarufu mara nyingi hutajwa sana kuhusishwa kwenye mijadala mingi mtandaoni humo. Hivyo Twitter huhesabu na kuweka takwimu vizuri zinazoonesha utajo wako kuanzia ndani ya siku saba na mwezi mmoja (siku 28)

  1. Omba Tweet Maps
    Tweet map ni muhimu sana. Hii itakuwezesha kufahamu wafuasi (followers) wako wanapatikana katika maeneo gani duniani na katika hili Twitter huonesha kwa asilimia kabisa. Fikiria unataka kufanya biashara kwa Watanzania, lakini akaunti unayonunua ina wafuasi laki Moja (100,000) mathalan, lakini kati ya hao zaidi ya 70% ni watu wa nje ya Tanzania. Kwa kigezo hiki hakika lengo lako la kibiashara inaweza kuwa ngumu kutimia hivyo zingatia hilo pia.
error: Content is protected !!