Tamko la familia ya Mtanzania aliyeuawa Marekani

HomeKitaifa

Tamko la familia ya Mtanzania aliyeuawa Marekani

Familia ya kijana Mtanzania Humphrey Magwira (20) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na Ramon Vasquez (19) nchini Marekani imesema kwamba kijana wao hakustahili kupoteza masiha hivyo haki itendeke dhidi yake.

Mama mzazi wa Humphrey anayeishi Houston amesema mtoto wake hakustahili kifo na kusisitiza kwamba enzi za uhai wake mwanae huyo alikuwa rafiki yake mkubwa na kifo hicho ni pengo kwa familia.

Mtuhumiwa wa mauaji hayo, Ramon bado yupo kizuizini ingawa polisi wametangaza dhamana ya dola za Marekani 500,000 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 1.152.

    > Kijana Mtanzania alivyouawa kwa risasi Marekani

Tangu kaka wa marehemu aanzishe kampeni ya kuchangia kusafirishaji wa mwili, wachangiaji zaidi ya 460 wamechangia zaidi ya shilingi milioni 52.45 na bado kampeni hiyo inaendelea kupitia mtandao wa ‘GoFundMe’ na simu (0715447436 na 0754447436) zote zimesajiliwa kwa jina la Janet Kuyangana.

Mama mdogo wa marehemu amesema mazishi yatafanyika Morogoro na kwa sasa msiba upo nyumbani kwao Kijitonyama jirani na Kanisa la TAG au njia ya Mesuma Hotel, Dar es Salaam.

error: Content is protected !!