Mganga abaka ili apate mbegu za kutengeneza dawa

HomeKitaifa

Mganga abaka ili apate mbegu za kutengeneza dawa

Mganga mmoja kutoka Chakechake, Zanzibar amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela ya kulipa fidia ya shilingi milioni 1 kwa kosa la kumbaka mke wa rafiki yake kwa madai kuwa zilikuwa zinahitajika mbegu za kiume kwa ajili ya kutengenezea dawa.
 
Kabla ya kufanya tukio hilo Issa Abdallah Haji (41) huyo alikuwa rumande kwa kosa la wizi ambapo alikutana na rafiki yake ambaye alipelekwa kwa kosa la wizi wa kutumia silaha ndipo baadae mganga alitoka nje kwa dhamana.
Baada ya kutoka rumande mganga alienda kwa mke wa rafiki yake huyo na kumwambia anataka amfanyie dawa ili mumewe atoke gerezani ila anatakiwa aende na nywele zake za sehemu ya siri pamoja na mbegu za kiume ambazo atazipata endapo watafanya mapenzi.
 
Mganga huyo alimwaminisha mke wa rafiki yake huyo kwamba angemtoa mumewe gerezani na ndipo Oktoba 11 alitekeleza tukio hilo la ubakaji.
 
Alifunguliwa mashtaka kutokana na kosa hilo kuwa kinyume na kifungu cha 108 (1), (3), (d) na 109 (1) sheria ya adhabu, sheria nambari 6 ya mwaka 2018 ya Zanzibar.
error: Content is protected !!