Uchambuzi mfupi wa album mpya ya Alikiba (Only One King)

HomeBurudani

Uchambuzi mfupi wa album mpya ya Alikiba (Only One King)

Mfalme wa Bongo Fleva nchini, Ali Kiba ameachia rasmi albamu yake ya 3 iliyokuwa inasubiriwa kwa muda mrefu yenye nyimbo takribani 16 aliyoipa jina la Only One King akidhihirisha kuwa katika muziki wa bongo fleva yeye ndiye mfalme wao.

Albamu hiyo imetayarishwa na Yogo Beats ambaye anaeleza kwamba ni heshima kubwa kufanya kazi na Alikiba huku akimshukuru kwa kumpa nafasi yakutayarisha nyimbo zote kwenye albamu hiyo.

Alikiba wamewashirikisha wasanii 3 kutoka Kenya (Khaligraph Jones, Sauti Sol na Nyashinski), watatu pia kutoka Nigeria (MayorKun, Rude Boy na Patoranking), mmoja kutoka Ghana (Sarkodie), mmoja kutoka Afrika Kusini (Blaq Diamond) na wengine ni kutoka kwenye label yake ya Kings Music (Tommy Flavour, Abdu Kiba, na K2GA).

Nakusogezea uchambuzi mfupi wa nyimbo zilizopo kwenye albamu hiyo ya Only One King;

1. Ayaya
Ndani ya wimbo huu Alikiba anaonesha  jinsi anavyomsifia mpenzi wake na kujidai uwe na mpenzi wake kwenye maisha yake.

2. Amour
Sifa nyingi zinamwagwa kwa mpenzi wake ndani ya wimbo huo, na ni kati ya nyimbo ambazo hazichoshi kusikiliza.

3. Tamba
Tommy Flavour, Abdu Kiba, K2GA wakali kutoka Kings Music wameutendea haki wimbo huu unaohusu kumshukuru Mungu kwa ajili ya mke bora.

4. Jealous
Ndani ya wimbo huu Alikiba na Mayorkun wanawaambia wapenzi wao wasiwe na wivu kwani wapo peke yao.

5. Sitaki Tena
Hapa  Alikiba anamwambia aliyewahi kuwa mpenzi wake kwamba hataki tena kurudi nyuma baada ya wao kuachana sababu ya kile anachodai kumsababishia maumivu moyoni.

6. Salute
Rude Boy na Kiba wanatoa pongezi na shukrani kwa wapenzi wao baada ya wao kwenda vitani na kupitia magumu lakini bado walibaki nao.

7. Washa
Akiwa na mwanaHipHop kutoka Kenya, Nyashinski wanawasihi wapenzi wao kuachana na maneno ya watu na kuzidisha mapenzi.

8. Infidele
Kwa kutumia lugha ya Kiingereza Alikiba anamwambia mpenzi wake anayemletea vituko na mikasa bora aende abaki peke yake kwani amechoshwa na mambo yake.

9. Bwana Mdogo
Uwepo wa mkali wa muziki kutoka nchini Nigeria, Patoranking umekamilisha wimbo huu mzuri unaohusu kumsifia mpenzi wake na kumwambia aachane na yale yanayosemwa na walimwengu.

10. Habity
Alikiba anatubu kwa mpenzi wake kwa kumwambia asiwe na wasiwasi kwani ni yupo peke yake huku  mkali wa Hip Hop kutoka nchini Kenya, Khaligraph Jones akikamilisha ladha nzuri ya wimbo huo.

11. Gimme Dat
Ni kati ya nyimbo ambazo ikipigwa kwenye kumbi za starehe basi bila shaka watu watasimama kwa kuwa unahusu jinsi Ali anavyomsifia mpenzi wake pale anapocheza kwenye moja ya kumbi za starehe.

12. Niteke
Alikiba ameamua kwenda mbali zaidi na kumshirikisha msanii kutoka nchini Afrika Kusini, Blaq Diamond kwenye wimbo huu ambapo wawili hawa wanaeleza jinsi gani wanawapenda wapenzi wao na wapo tayari hata kutekwa.

13. Let Me
Kwa mara ya pili sasa Alikiba anawashirikisha Sauti Sol kwenye nyimbo zake na kutoa wimbo mzuri ambapo kwa pamoja wanawaambiwa wapendwa kwamba wapo tayari kuwa nao.

14. Utu
Ndani ya wimbo huu Ali Kiba anaweka wazi ukweli kuhusu kile kilichomfanya ampende mpezni wake akisema kwamba amebarikiwa Utu.

15. Ndombolo
Kwa mara nyingine tena wasanii kutoka Kings Music wameungana na kuonesha jinsi gani wanaweza kucheza ndombolo.

16. Happy

Katika wimbo huu ambao amemshirikisha Sarkodie kutoka nchini Ghana, Alikiba anamwimbia mwanamke ambaye anampenda na anataka awe mpenzi wake kwani wote wawili wamepangwa kuwa pamoja, na umoja huo utomfanya awe mwenye furaha.

error: Content is protected !!