Historia: Mtanzania ashinda Tuzo ya Nobel

HomeKimataifa

Historia: Mtanzania ashinda Tuzo ya Nobel

Tuzo za Nobel katika Fasihi (Nobel Prize in Literature) imetolewa leo na kushuhudia Mtanzania Abdulrazak Gurnah, akishinda tuzo hiyo.

Abdulrazak Gurnah ni Mtanzania aliyezaliwa huko Zanzibar mwaka 1948. Miaka ya 1960 alikwenda Uingereza ambako alipata nafasi ya kusoma.

Amewahi kuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha Bayero nchi na Nigeria, na sasa pamoja na uandishi wa vitabu ni Profesa katika chuo kikuu cha Kent nchini Uingereza.

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete

Ameshinda tuzo hiyo kutokana na jinsi kazi zake za fasihi tangu aanze uandishi, zilivyoweza kugusa maisha, zikiangazia athari za ukoloni na maisha ya ukimbizi.

Tuzo hiyo ambayo imeambata na zawadi ya fedha zaidi ya shilingi bilioni 2.6 kwa fedha za Kitanzania, inamuweka Mtanzania huyo kwenye historia ya kutwaa tuzo hiyo ambayo Mwafrika wa mwisho kuipata alikuwa Wole Soyinka wa Nigeria (1986).

error: Content is protected !!